Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe.Ibrahim Ngwada amesema ili kukamilisha ujenzi wa Machinjio ya Ngelewala iliyopo Manispaa ya Iringa inahitajika fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.9 hivyo amemuomba waziri Mkuu mstafu Mhe.Mizengo Peter pinda kusaidia upatikanaji wa fedha hizo na Machinjio hiyo iweze kufanya kazi kisasa.
Ngwada ameyasema hayo Februari 8,2023 wakati wa ziara ya Waziri Mkuu mstaafu Mhe.Mizengo Pinda ya kutembelea na kukagua mradi huo ambao ulianza kutekelezwa mwaka 2008 na kugharimu jumla ya sh..bilioni 2.2 mpaka sasa
Mhe.Ngwada amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa Machinjio hiyo na kusema kuwa mradi huo ukikamilika utaongeza uchumi wa Halmashauri na wananchi wake.
Kwa upande wake Mizengo pinda amesema amejionea hatua iliyofikiwa katika machinjio ya Ngelewala na kupongeza uongozi wa Manispaa kwa usimamizi mzuri na kuahidi kuwa ataungana na viongozi wa ngazi ya juu kuhakikisha fedha hizo zinapatikana na kumalizia ujenzi wa Mradi huo mkubwa wa kimkakati.
Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Dr.Stephen Ngwale amesema kukamilika kwa machinjio hiyo kutaongeza ajira kwa vijana zaidi ya 400.,kuongeza mapato ya Halmashauri na kukuza uchumi wa wananchi wa Manispaa.
Ziara hiyo ya siku moja iliwahusisha viongozi mbali mbali wa Chama na Setikali Mkoa wa Iringa akiwepo Mkuu wa Mkoa Mhe.Halima Dendego.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa