Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard Kasesela amewataka viongozi wapya wa bodi ya huduma za Afya ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kutimiza wajibu wao kwa kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo ili jamii iweze kupata huduma bora.
Kasesela ameyasema hayo katika kikao cha uzinduzi wa bodi mpya ya Halmashauri ambacho alikuwa mgeni rasmi,kilichofanyika tarehe 27/11/2020 katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa.
Ndugu Hamid Njovu ni Mkurugenzi wa Maniaspaa ya Iringa aliwapongeza mwenyekiti na katibu kwa kuchaguliwa kuongoza bodi hiyo kwa miaka mitatu na kuwataka kuangalia changamoto za sekta ya Afya zilizoko hasa katika maeneo ya pembezoni kama vile kata ya Nduli,Kitwiru na Isakalilo eneo la Mkoga kuhakikisha maeneo hayo yanapata zahanati na vituo vya Afya.
Nae Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Bi.Jesca Lebba amebainisha lengo la kuanzisha bodi na kamati hizo ni ushirikishwaji wa Jamii pamoja na ushirikiano na sekta zingine katika kuboresha sekta za Afya.
Aidha Dr. Lebba amesema bodi za huduma za afya za Manispaa zimeundwa chini ya sheria ya serikali za mitaa ( Mamlaka ya Wilaya) sura Na. 287,Sheria ya Serikali za mitaa (Mamlaka ya Miji) sura Na.288,na Hati rasmi iliyopitishwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na kutangazwa kwenye gazeti la Serikali.
Katika kikao hicho Dr.Benedict Ndawi alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa bodi na Bi.Nina pope.
alichaguliwa kuwa katibu.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa