Mwelekeo wa afya ya akili Duniani unazidi kutia shaka ambapo wataalam wa afya wanajitahidi kuongeza bidii ili kubadili mtazamo wa watu, tiba na hatua dhidi ya chanzo cha tatizo la afya ya akili ikiwemo matibabu.
Kutokana na tatizo hilo kuonekana kuwa kubwa likiathiri sana kundi la vijana viongozi mbalimbali, wakiwemo viongozi wa Serikali na dini wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha jamii inaelimishwa kuhusu tatizo hilo.
Akizungumza katika sherehe za mahafali ya 52 ya shule ya Sekondari ya wasichana Iringa, Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini, Mkoani Iringa, Dkt. Jesca Msambatavangu pamoja na masuala mengine amezungumzia suala la afya ya akili kama tatizo kubwa hivi sasa linaloiathiri jamii hasa vijana ambao baada ya kuhitimu elimu zao wanajikuta wakipata msongo wa mawazo baada ya kukosa ajira
Aidha Mbunge huyo amezungumzia pia suala la nafasi ya mwanamke katika jamii kuweza kupambana na changamoto mbalimbali, ikiwemo kushiriki shughuli za ujasiriamali ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuondoa dhana ya utegemezi kwa familia.
Katika sherehe hiyo Mbunge huyo aliendesha zoezi la harambee ya ujenzi wa bweni la mshikamano harambee iliyowahusisha wazazi na wageni waalikwa ambapo jumla ya Tsh 731,000 zilipatikana papo hapo huku Mbunge aliahidi kuchangia Tsh 1,500,000 na Diwani wa Kata ya Gangilonga mhe.Lenyata Likotiko aliahidi kutoa kiasi cha Tsh 500,000 na hivyo kufanya jumla ya michango yote kufikia kiasi cha Tsh 2,731,000.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa