Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Veronica Kessy amezitaka timu zilizopangwa kwa ajili ya kutoa chanjo sehemu mbalimbali, zijipange ipasavyo ili ziweze kuwafikia walengwa wote pasipo kukosa.
Kessy alizungumza maneno hayo leo tarehe 15/02/2024 katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo wakati akifungua mkutano wa kampeni ya utoaji chanjo ya Surua Rubella kwa watoto wa kuanzia miezi tisa mpaka chini ya miaka mitano, ambayo itafanyika kwa siku nne kuanzia leo tarehe 15.02.2024 mpaka tarehe 18.02.2024 itakapohitimishwa.
Aidha aliwasihi wataalamu wa afya waliokuwepo kutoka manispaa na halmashauri ya Iringa, kuhakikisha wanajipanga ipasavyo kuhakikisha zoezi la utoaji chanjo linafanikiwa kwa asimilia zote.
Wakati huohuo Kessy aliziomba taasisi za dini ziweze kuwahubiria waumini wao waweze kujitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo ya Surua Rubella inayoambukizwa kwa njia ya hewa kutokana na virusi viitwavyo Morbillivirus Paramyxoviridae.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa