Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Mohamed Moyo ametoa rai kwa wananchi kuepuka taarifa zozote za upotoshaji zinazohusu utolewaji wa huduma za Chanjo hususani chanjo ya UVIKO 19 kwani ni salama
Hayo ameyasema leo Oktoba 21, 2022 katika Mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Stendi ya Kidamali Kata ya Mwangata wenye lengo la kuhamasisha jamii juu ya uchanjaji wa chanjo ya Uviko 19
Hata hivyo Mhe. Moyo ameeleza kuwa kupitia mitandao ya kijamii na ushawishi wa ana kwa ana, kumekuwa na taarifa ambazo inasemekana ukipata chanjo hiyo basi kwa wanawake wanakosa kupata ujauzito lakini kwa wanaume kushindwa kufanya tendo la ndoa ipasavyo, jambo ambalo si kweli na hivyo kuwataka kupuuzia uzushi wa taarifa kama hizo
Sanjari na hayo amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya Uviko ambayo hutolewa bure bila malipo na ni kinga ya mwili itakayoepusha gharama kubwa endapo mtu akiathirika na ugonjwa huo na huweza kupelekea kifo.
Aidha mhe.Moyo amewashukuru shirika la HFI 360, Mashirika ya kiserikali na binafsi, watendaji pamoja na viongozi wa dini kwa juhudi wanazozifanya katika kuhakikisha zoezi hilo la utolewaji wa chanjo linaenda kwa ufanisi
Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Mwangata MheGalus Lugenge. amemshukuru Mkuu wa Wilaya kwa kufika katika eneo lake na kufanya hamasa hiyo na kuwaomba wananchi wajitokeze kupata chanjo hiyo ambayo ilikuwa ikitolewa eneo hilo
Kaimu Mganga Mkuu wa Manispaa ya Iringa Dr.Godfrey Mtunzi Iringa amesema walengwa wakupatiwa chanjo ni 123,418, mpaka kufikia sasa Halmashauri imefanuikiwa kuchanja watu 112,669 ikiwa ni sawa na asilimia 91% na kusema kuwa utolewaji wa elimu umesaidia wananchi wengi kujitokeza kupata chanjo hiyo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa