AAHIDI KUTOA SH BILIONI 1.9 KWA AJILI YA VIFAA VYA KISASA
Katibu Mkuu wa CCM Taifa ndugu.Daniel Chongolo ameahidi fedha kiasi cha sh.bilioni 1.9 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa Machinjio ya Ngelewala pamoja na ununuzi wa vifaa vya kisasa vitakavyotumika katika Machinjio hiyo iliyopo Kata ya Mwangata Manispaa ya Iringa.
Chongolo ameyasema hayo Juni 1 2023 alipokuwa akihitimisha ziara yake ya siku 7 Mkoani Iringa ambapo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ametembelea mradi wa mchepuo wa Barabara ya Tumaini- Igumbilo na upanuzi wa uwanja wa ndege Iringa ( Nduli)
'Nitawaita Dodoma Mkuu wa Mkoa, Mstahiki Meya, Mkurugenzi na.baadhi ya wataalam na viongozi wa chama na Serikali
Ili tuzungumze namna gani tunaweza kuinusuru machinjio hii kwa kupata fedha kiasi hicho kwa ajili ya ukamilishaji wa Machinjio hii ili iwe ya kisasa na ilete tija kwa Halmashauri na wananchi wa Manispaa na maeneo mengine alisema Chongolo."
Naye Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego amesema walikaa na Halmashauri nakufanya tathimini ya mradi huo wa Machinjio na kupata gharama zinazohitajika kukamilisha ujenzi pamoja na vifaa vya kisasa vya kuchinjia ambapo jumla ya sh.bilioni 1.9 zinahitajika kukamilisha mradi huo na zitatimiza ndoto zetu za kuwa kiwanda cha nyama na Machinjio ya kisasa Manispaa na Mkoani Iringa kwa ujumla.
Dendego amesema miradi inayokaa muda mrefu huwa na gharama kubwa kuikamilisha lakini lengo ni zuri na kwa kuwa Baba leo umekuja najua utasema kitu alisema Dendego.
Awali akisoma tariifa ya utekelezaji wa mradi huo Afisa Mifugo na Uvuvi wa Manispaa ya Iringa Dr.Stephen Ngwale amesema Mradi wa Machinjio ya Ngelewala ulianza rasmi kutoa huduma Julai 2022 kwa kutoa huduma ya uchinjaji Ng"ombe,Mbuzi na kondoo na inafanya kazi kwa mfumo wa kawaida.
Dr.Ngwale amesema mradi huo mpaka sasa umefikia wastani wa asilimia 95 na kuwa umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 2 na kuwa mradi huo kwa sasa unachinja Ng'ombe 30 hadi 40 ,Mbuzi 15 hadi 25, Kondoo 10 hadi 15. Kwa siku huku akibainisha mafanikio ya mradi kuwa ni utoaji wa ajira 172 kwa wakazi wa Manispaa na kuongezeka kwa mapato ya ndani ya Halmashauri kwani katika kipindi cha Julai hadi Aprili 2023 Machinjio hiyo imeiingizia Halmashauri zaidi ya shilingi milioni 60 ambazo zimekusanywa kama ushuru wa nyama.
Katika ziara hiyo Mhe.Jeca Msambatavangu Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini amemkaribisha Katibu Mkuu Ccm Taifa na kumuomba kuangalia suala la miundombinu ya Barabara ya kutoka Machinjio hadi kitasengwa kutokea Kalenga iweze kuboreshwa ili kupunguza adha kwa wakazi wa maeneo hayo hasa wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari Isakalilo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa