Mkuuwa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Veronica Kessy amewaomba Viongozi wa Dinikusaidia kutoa elimu ya maadili katika jamii ili kuacha vitendo vyaudhalilishaji na kuwa na hofu ya Mungu.
Mhe.Kessy amesema hayo alipokuwa mgeni rasmi wa siku ya Kilele cha maadhimisho ya SikuKumi na Sita za kupinga ukatili wa kijinsia kwa watoto, wanawake na wanaumeyaliyofanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kufanya matembezi yahiari huku yakiambatana na kuadhimisha miaka 62 ya Uhuru.
Hatahivyo Mhe. Kessy amelipongeza Jeshi la Polisi na Kitengo cha Dawati la Jinsia kwaushirikiano wanaotoa kwa matendo yasiyokuwa ya kibinadamu kwa kuwa vitendo hivoni ushetani.
Aidha amewataka waganga wa kienyeji kuacha kufanya lamli chonganishi ili watu wapateutajiri kwa kukata viungo vya watu wenye ulemavu wa ngozi, kulawiti na kufanyavitendo vya ngono kwa watoto wadogo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa