Na Mwandishi Wetu, Iringa
WATU wanne wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Isamilo kugongana na lori huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa lori.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mohamed Moyo, amesema ajali hiyo imetokea jana usiku Oktoba 27, mwaka huu katika kijiji cha Izazi kata ya Izazi tarafa ya Isimani wilayani Iringa barabara kuu ya Iringa -Dodoma .
Alisema basi hilo lenye namba za usajili T 398 BNH YUTONG lililokuwa likitokea Mwanza liligongana na lori la mizigo lenye namba T760BBY aina ya scani na kusababisha vifo vya watu wa nne na wengine wamejeruhiwa.
Moyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, alisema chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa lori kujaribu kuyapita magari yaliyokuwa mbele bila kuchukua tahadhari na dereva huyo baada ya ajali alikimbia.
Aliongeza kuwa lori hilo la kampuni ya Justas Investment Co limited lilikuwalikitokea Iringa wakati basi hilo lilikuwa likitoka Mwanza kwenda Mbeya lilikuwa likiendeshwa na Emmanuel John Ng'wiguka (49) mkazi wa Buzuruga Mwanza .
Mkuu huyo wa wilaya aliwataja waliofariki katika ajali hiyo kuwa mi Gerald John ambae ni dereva wa Mwanza, Happy Kwangu ambae ni utigo na mkazi wa Bunda, Edga ambae ni utingo mkazi wa Nyamongo Mara na abiria mmoja ambae bado hajafahamika jina jinsia ya kiume.
Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa na majeruhi wanaendelea na matibabu katika Hospitali hiyo .
Majeruhi wa ajali hiyo ni Ngeleja Mlima (36) mkazi wa Geita, Allen Gahanga (21) mkazi wa Mwanza, Sprime Kitanda (35) mkazi Igunga, Fredrick Mgalula (36) mkazi wa Mafinga, Charles Mashauri (23) mkazi wa Mwanza, Novat Isaya (23) mkazi wa Igunga na Paulo Kayuki (25) mkazi wa Kalenga .
MWISHO
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa