Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesera ametembelea na kukagua ujenzi wa madarasa na Shule mpya zitakazo wapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza ifikapo Januari 11. 2021, Manispaa ya Iringa
Mh. Kasesela ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Manispaa kuwa shule hizo na madarasa ambayo hayajakamilika, kushughulikiwa haraka ili kuondokana na adha mara baada shule kufunguliwa
Akizungumza na wazazi wa Kata ya Nduli wakati wa ukaguzi Shule ya Sekondari ya Nduli amewataka kuhamasisha na kuwaleta watoto wote shuleni waliofaulu na sio kuwaacha kutangatanga mitaani
Hayo ameyasema kutokana na kasumba ya wazazi walio wengi kushindwa kuwasomesha watoto wao bila kuwa na sababu za msingi
Hata hivyo ameipongeza Halmashauri kwa jitihada kubwa iliyofanyika katika kutatua tatizo la upungufu wa madarasa, huku akiitaja sababu moja wapo iliyowakwamisha kumaliza ujenzi kwa wakati ni uwepo wa janga la ugonjwa wa Covid 19
"Niwapatie wiki moja kukamilisha miradi hiyo na mara baada ya hapo nitapita tena kukagua" Kasesela aliongezea
Sambamba na hilo Mh. Kasesela ameilaumu kampuni ya Cocacola kwa kushindwa kutimiza ahadi yake ya ujenzi wa kiwanja cha mpira wa Miguu cha shule ya Sekondari kihesa waliyoahidi katika shindano la kuokota makopo lililohusisha shule mbalimbali za Manispaa ya Iringa
Nae Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Hamid Njovu amemshukuru Mh. Mkuu wa Wilaya kwa kutembelea miradi hiyo na kumuahidi kuikamilisha haraka kwa muda uliobakia
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa