Katika kuadhimisha siku ya wazee duniani Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupitia ofisi ya Ustawi wa jamii imetoa elimu mbalimbali kwa wazeee pamoja na upimaji wa afya zao bure.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela amewataka wahudumu wa afya kuwapa kipaumbele wazee na kutumia lugha nzuri pindi wanapo wahudumia.
Awali mganga Mkuu wa Manispaa ya Iringa Bi. Jesca Leba amesema maadhimisho hayo ni muhimu kwa wazee kupata elimu mbalimbali kuhusiana na afya zao na kupitia idara ya afya ya Manispaa kuhakikisha wazee wanapata haki zao za msingi na kuishi maisha bora.
Kwa upande wake Afisa lishe kutoka Manispaa ya Iringa Bi. Nzaeli Benet amewataka wazee kula mlo kamili kutoka katika makundi matano ya vyakula kama matunda, maziwa, mboga za majani ambavyo vitaboresha afya zao Kwani kadiri umri unavozidi kwenda wazee wanazidi kukumbana na matatizo mengi kiafya kutokana na lishe duni.
Katika risala yao Wazee wameitaka jamii kuwaheshimu wazee na kutambua mchango wao katika kuleta maendeleo yao na Taifa kwa ujumla pamoja na kutambua kuwa utu uzima ni dawa.
Aidha wazee hao wamepatiwa vitambulisho vya matibabu bure, elimu ya lishe, elimu ya mpiga kura, elimu ya bima ya Afya ya jamii,elimu ya ustawi wa wazee pamoja na upimaji wa BP na BMI.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa