Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Iringa ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Veronica Kessy imefanya ziara ya kutembelea na kukagua Miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa ya Iringa Agosti 17.2023.
Aidha Miradi iliyotembelewa na kukaguliwa katika ziara hiyo ni pamoja na Upanuzi wa uwanja wa Ndege Nduli,Jengo la V.IP Hospitali ya Mkoa,Barabara ya Mchepuko ya Tumaini Igumbilo,Ujenzi wa wodi na jengo la watoto Hospitali ya Wilaya Frelimo na Soko la Machinga Mlandege
Katika ziara hiyo Mhe.Kessy amemtaka kaimu Mkurugenzi ndugu Charles Mwaitege kusimamia miradi hiyo ili ikamilike kwa wakati na iweze kutumika na kuleta tija kwa wananchi pia amesizitiza ujenzi huo uendane na thamani ya fedha zilizotolewa.
Wakati huo huo Kamati imejionea maboresho yanayoendelea ujenzi wa Miundo mbinu ya Barabara, Maji na Umeme katika Soko la Machinga Mlandege ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe.Halima Dendego mara baada ya kupokea maombi kutoka kwa wafanyabiashara wadogo Machinga katika kikao chake na Machinga kilichofanyika tarehe 10 Agosti Katika Ukumbi wa Mercy Hall Uliopo Kata ya Mlandege.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa