Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Kheri James awashauri na kuwahimiza vijana wa mapinduzi wilaya Ya Iringa mjini, kujenga mshikamano miongoni mwao na kuwajibika ipasavyo katika ujenzi wa jumuiya na shughuli zao za uzalishaji mali.
Komredi kheri ameyasema hayo wakati akiwasilisha salamu zake katika kikao cha baraza la vijana cha chama cha mapinduzi kilichofanyika katika ofisi za CCM wilaya Iringa mjini.
Akizungumza katika kikao hicho, ameeleza kuwa umoja na mshikano ni silaha muhimu saana katika safari ya kuyafikia mafanikio,kwahio ni muhimu vijana wakaendelea kushikamana na kushirikiana katika kusimamia ajenda zinazowagusa vijana wote kwa ujumla.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na viongozi wa chama, jumuiya na wadau mbalimbali wa maendeleo ya vijana katika wilaya ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa