Mkuu wa Wilaya ya Iringa mhe.Mohamed Moyo leo tarehe 23/6/2021 amekutana na kuzungumza na wazee wa Manispaa kwa lengo la kufahamiana na kusikiliza changamoto mbalimbali zinazo wakabili na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka
Mhe. Moyo amesema amepokea changamoto zao na atazifanyia kazi mara moja na kuwaomba wazee waendelee kukiamini chama cha Mapinduzi kwani kinawathamini wazee sababu wao ni tunu ya Taifa letu
Aidha amesema ameweka mkakati wa kukutana na wazee kila baada ya miezi mitatu kuwapa mrejesho wa utekelezaji wa changamoto walizo zitoa na kuwasikiliza na kujadiliana masuala ya maendeleo ya Manispaa
Changamoto walizotoa wazee katika kikao hicho ni pamoja na usumbufu wanaoupa kwenye vituo vya afya na zahanati kutokupewa kipaumbele wanapohitaji huduma za afya, changamoto za mfumo katika kupokea fedha za TASAF,miundombinu ya barabara kuwa mibovu pia kituo cha Polisi Semtema kutokufanya kazi masaa ishirini na nne(24)
Mhe.Ibrahimu Ngwada ni Mstahiki Meya Manispaa amesema Halmashauri imeshanza kutatua kero hizo na tayari matengenezo ya baadhi ya barabara yanafanyika pia hatua za kufanya kituo cha polisi cha Semtema kufanya kazi masaa ishirini na nne iko kwenye utekelezaji
Kikao hicho kilihudhuriwa na wazee, viongozi wa chama na Serikali ambapo wazee wameonesha furaha yao kwani wamekuwa kundi la kwanza kukutana na Mkuu huyu mpya wa Wilaya.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa