Mkuu wa wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Moyo amewapongeza Idara ya afya kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuhamasisha jamii kujitokeza kwa wingi katika chanjo mbalimbali zinazotolewa kwa watoto .
Moyo ametoa pongezi hizo katika kikao cha kamati ya Afya ya msingi (PHC) kilichofanyika leo Novemba 29 katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa.
'Nawapongeza sana Idara ya Afya Manispaa kwa kazi kubwa na nzuri mnayoifanya ya utekelezaji wa kampemi mbalimbali kama ugawaji dawa kinga za minyoo na kichocho na chanjo ya matone kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mi 5 mmekuwa mkinialika kuzindua kampeni mbalimbali hakika naona muitikio wa jamii unakuwa mkubwa,alisema Moyo.
Juhudi zenu zina manufaa kwa wakazi wa Manispa na Taifa kwa ujumla kwani mnaokoa nguvu kazi ya Taifa la kesho.
Awali akitoa mada katika kikao hicho Mratibu wa Chanjo Manispaa ya Iringa Ndg.Hamis Omary amesema Halmashauri ya Manispaa ya Iringa inaungana na Halmashauri zingine nchini kutekeleza awamu ya nne (4) ya utoaji wa chanjo ya polio ya matone kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 itakayofqnyika kuanzia tarehe 1 hadi 4 Disemba.
Omary amesema lengo la kampeni ya kitaifa ya chanjo ya matone ya polio ni kuhakikisha wanazuia uingizwaji wa ugonjwa wa polio nchini kulingana na mlipuko uliotokea nchi za Malawi na Msumbiji.
Amesema ili kufanikisha lengo hili ni muhimu kutoa kinga ya polio kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mi 5.
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Iringa Dr.Godfrey Mbangali amesema awali Halmashauri imetekeleza kampeni ya utekelezaji wa chanjo kwa awamu mbili .
Amesema matokeo ya kampeni ya awamu ya pili iliyotekelezwa mwezi Mei 2022 walilenga kuchanja 23.675 na waliochanjwa walikuwa 29.887 sawa na asilimia 126.2 ambapo awamu ya tatu iliyotekelezwa Agosti 2022 walengwa walikuwa 30,781 waliochanjwa 35,880 sawa na asilimia 116.6
Kikao hicho cha kamati ya Afya yamsingi kilihudhuriwa na wajumbe ambao ni kamati ya ulinzi na usalama Wilaya, wakuu wa Sehemu na Vitengo,,baadhi ya Madiwani, Viongozi wa dini na watu maarufu.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini -Iringa Mc
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa