Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Mohamed Moyo amewataka walimu wakuu,wakuu wa Shule, Maafisa Elimu Kata,wadhibiti ubora wa Shule na Tsc wa Halmashauri ya Manispaa ya iringa, kuhakikisha wanatekeleza vyema maagizo ya Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya miongozo ya Elimu ya Msingi na Sekondari.
Mhe. Moyo ameyasema hayo leo 21/8/2022 katika hafla fupi iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Manispaa alipokuwa akizindua vitabu vitatu( 3) vyenye lengo la kuimarisha usimamizi wa utolewaji wa Elimu, Mhe Moyo amewataka kwenda kutekeleza miongozo hiyo kwa vitendo ili kuleta tija katika Sekta ya Elimu Msingi na Sekondari.
Akitoa taarifa ya miongozo hiyo mitatu Afisa Elimu Sekondari Bi.Tupe Kayinga amesema miongozo iliyozinduliwa ni Uteuzi wa viongozi wa Elimu, Kuboresha Elimu, Changamoto za Elimu na utatuzi wake.
Awali Mhe. Moyo amewapongeza wakuu hao wa shule, walimu wakuu,waratibu Elimu Kata kwa namna ambavyo wanasimamia vyema majukumu yao katika Sekta ya Elimu hali inayoifanya Iringa kuzidi kung'ara katika ufaulu wa wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari kwa Mwaka 2021 na amesema anaimani miongozo hiyo itakuwa chachu ya kuleta matokeo mazuri zaidi kwa mwaka 2022.
Kwa Upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada ametoa ahadi kwa mara nyingine ya kutoa zawadi ya gunia moja la mchele na fedha kiasi cha shilingi laki tano (5) kwa Shule itakayofanya vizuri katika somo la Hisabati ambapo zawadi hizo atapewa Mwalimu Mkuu pamoja na Mwalimu wa somo la Hisabati.
Aidha Ngwada anewataka walimu kuongeza juhudi katika ufundishaji ili kuwa na matokeo mazuri zaidi kwa mwaka 2022 huku akiahidi kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndg. Gerald Mwamuhamila amemshukuru Mkuu wa Wilaya ya Iringa kwa kuhudhuria zoezi hilo la uzinduzi na kuahidi kushirikiana vyema na walimu hao ili kuhakikisha lengo la uzinduzi huo la kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao linatimia.
Akihitimisha Mhe. Moyo amekemea tabia ya baadhi ya walimu kushiriki vitendo viovu vya unyanyasaji kwa wanafunzi hali ambayo huweza kupelekea kushindwa kufanya vizuri katika masomo yao.
Uzinduzi huo umehudhuriwa walimubwakuu,Wakuu wa shule,waratibu Elimu, Kata,watendaji wa Kata, wathibiti ubora wa Elimu,wakuu wa Sehemu na vitengo pamoja na baadhi ya waheshimiwa Madiwani.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO-MANISPAA YA IRINGA.
@halimadendego
@mohamedmoyo
@ortamisemi
@maelezonews
huhuhuhuhuhu
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa