Jamii imetakiwa kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa uviko -19 kwa kuchanja ili kujiepusha na ugonjwa huo hatari duniani kote.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa wilaya ya Iringa mhe.Mohamed Moyo wakati akiongea na wananchi wa Kata ya Gangilonga katika mkutano wa hadhara mara baada ya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa katika Manispaa ya Iringa.
Moyo amesema watu wengi wanaogopa kuchanja kujikinga na uviko 19 kwa kuhofia kuwa mazombi kama ambavyo imekuwa ilipotoshwa na baadhi ya watu wasioitakia mema nchi yetu ya Tanzania.
Katika hatua nyingine mhe Moyo amewapongeza wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa shule ya sekondari wasichana Iringa,Lugalo , Mlamke na Mkwawa kwa juhudi kubwa wanayoifanya kwani wamepiga hatua kubwa hivyo kuleta imani ya kukamilisha miradi hiyo kwa wakati uliopangwa.
Mhe Moyo amewapongeza wazazi/walezi na walimu kwa kazi nzurri waliyoifanya kuhakikisha wanafunzi wa darasa la saba wamefaulu kwa kwango cha juu kwani Mkoa wa Iringa umekuwa wa pili Kitaifa katika ufaulu wa Wanafunzi wa darasa la saba kwa mwaka 2021.
Ziara hiyo ya Mkuu wa wilaya ya Iringa inayojulikana kama Ulipo nipo imeanza leo Manispaa ya Iringa ambapo ametembelea na kukagua miradi ya maendeleo na kupokea kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Omary Mkangama ni kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na atayafanyia kazi haraka kwa manufaa ya wananchi wa Manispaa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa