Na Mwandishi Wetu, Iringa
MKUU wa Wilaya ya Iringa, Mohamed Moyo pamoja na viongozi wengine wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wameadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania kwa kushiriki ujenzi wa madarasa katika shule ya Sekondari Kleruu iliyopo kata ya Gangilonga yanayojengwa kwa fedha za UVIKO-19.
Mhe.Moyo alishiriki zoezi la ujenzi wa madarasa akishirikiana na Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa mhe.Kenyata Likotiko ambaye pia ni diwani wa kata ya Gangilonga, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa ndugu Limbe B.M Limbe, wakuu wa idara na vitengo na baadhi ya watumishi wa manispaa.
Mheshimiwa Moyo amesema si rahisi nchi kusherekea uhuru wa miaka 60 lakini kwa Tanzania imewezekana kutokana na upendo, amani na utulivu tulionao.
"Watanzania tumejifunza uvumilivu ambao umepelekea nchi yetu kuwa huru na watu wake kufurahia uhuru huo," alisema Moyo.
Mkuu huyo wa wikaya aliwaomba Watanzania wote kusherehekea maadhimisho hayo kwa amani na utulivu
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa