Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe. Halima Dendego ameongea na wafanyabishara wote katika Mkutano mkuu wa mwaka wa wafanyabiashara wa Iringa tarehe 7 Dec, 2023, katika ukumbi wa Royal Palm uliopo Iringa mjini.
Dendego aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya wa Iringa mjini Mhe. Veronica Kessy, aliwataka wafanyabiashara wote kwa umoja wao wawe watulivu kwenye maeneo yao rasmi ya kufanyia biashara ili iwe rahisi kwa serikali kuona jinsi gani wataweza kuwasaidia na kwa pamoja kuikuza sekta hio kwan anatamani wafanyabiashara waweze kufanya biashara zao saa 24.
“Zanzibar wameanza na wameweza na sisi wafanyabiashara wa Iringa tunataka tuwe wa kwanza Tanzania Bara kufanya biashara masaa 24 haswa upande wa masoko, badala ya kufunga biashara zetu saa 12 jioni.”
Mkuu wa Mkoa aliendelea kuwasihi wafanyabiashara hao waliokua wamefurika kwa wingi, kuwa wahakikishe wanalipa kodi kwa serikali na wawe wepesi kutoa risiti kwa wateja wao, kwani kodi ni uzalendo na ni muhimu kwa serikali katika kuleta maendeleo ya sehemu husika.
Aidha aliwashukuru kwa ushirikiano wao wanaoonyesha kwa kufuata na kutii maelekezo mbalimbali yanayotolewa na serikali, kwani kwa kufanya hivyo inaonyesha ukomavu uliopo na hii inapelekea kuzidi kuboresha Zaidi sekta ya biashara.
Mwisho kabisa Dendego alitoa rai kwa wafanyabiashara hao kuchangisha na kumuunga mkono Rais Dr Samia Hassan Suluhu kwa kuweza kutoa kiasi chochote kile walichonacho kwa ajili ya wenzetu waliokumbwa na maafa ya mafuriko huko Hanangi Mkoani Manyara, ambapo wafanyabiashara hao waliweza kuchanga papo kwa papo na wadau wenginge kutoa ahadi ya fedha, chakula n.k.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa