Mkuuwa Mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amewaasa wafanyabiashara kuyajali maeneoyao wanayofanyia biashara kwa kuyatunza na kuepuka ujenzi holela wa vibandavichochoroni na mbele ya maduka yao.
Mhe.Dendego amesema hayo Novemba 21, 2023 akiwa Soko la Mashine Tatu katikamuendelezo wa operesheni ya usafi yenye kauli mbiu ya “Iringa Uchafu Sasa Basi”ikiwa ni siku ya pili tangu kuanza na kupata fursa ya kuzungumza nawafanyabiashara wa eneo hilo akiwaasa kuyajali maeneo yao kwani tatizolinapotokea ni ngumu kwa maeneo hayo kupitika na kutoa msaada kwa haraka.
"Kufanyabiashara holela kunasababisha mlundikano wa watu katika eneo moja kitu ambachoni hatari, hivyo tufuate maelekezo kutoka serikalini na pia nisione mtuanajenga vibanda tena sehemu za vichochoroni, wala kufanya biashara mbele yaduka la mtu, ninachotaka maeneo yote yawe wazi ili yaweze kupitika kwa urahisina mji upendeze" Amesema Dendego
Operationya "Iringa Uchafu Sasa Basi" imeongozwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. HalimaDendego aliyeambatana na Mkuu wa Wilaya Mhe. Veronica Kessy pamoja na Mkurugenziwa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Ndg. Kastori Msigala na Mbunge wa IringaMjini Mhe. Jesca Msambatavangu.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa