“Iringa mwaka huu msiniangushe huwa mnaniumiza sana, tunapata shida kupata connection, ukikosa connection hakuna maendeleo, hapa hakuna connectin, Nileteeni Jesca Muone yatakayotokea Iringa” JPM
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na mgombea Urais kupitia chama hicho dkt.John Pombe Magufuli amewaomba wana Iringa kumpa kura nyingi za ndio ili kukamilisha mambo mengi yaliyomo kwenye ilani ya Chama cha Mapinduzi(CCM)
Akizungumza katika viwanja vya Samora leo Dr..Magufuli amesema iwapo atapewa nafasi nyingine ya kuiongoza Tanzania atafanya maajabu kwa kuubadilisha Mkoa wa Iringa.
“Tupate viongozi watakaoulinda Muungano wetu, ni ccm pekee ndiyo yenye kuleta usawa bila kubagua itikadi za vyama,dini na makabila”.
Naye Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Iringa Mh. Mizengo Pinda amemuhakikishia Mh. Magufuli kuwa CCM itashinda kwa kishindo Mkoani hapa kwani wamejipanga kuanzia ngazi ya shina mpaka Taifa.
Kwa upande wake mgombea Ubunge jimbo la Iringa Mjini kupitia chama cha Mapinduzi Ndg.Jesca Msambatavangu amesema kuwa akichaguliwa kuwawakilisha wananchi wa jimbo la Iringa mjini atahakikisha changamoto zote zinafanyiwa kazi ikiwemo ukarabati wa masoko pamoja na kupunguza ushuru kwa wafanyabiashara wadogo .
Aidha mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama na serikali,wananchi wa vyama mbalimbali, wagombea Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi Mkoani ,wagombea udiwani ambao walipata nafasi ya kumuombea kura Mwenyekiti wa chama hicho pamoja na kujiombea kura nyingi za ndio wao wenyewe.bila kusahau wasanii walipata fursa ya kutumbuiza katika mkutano huo akiwemo mwanamuziki nguli Hamonize kuwafanya wanachi kulipuka Kwa shangwe,vigelegele na nderemo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa