"Ipo haja ya kuendelea kutoa elimu ya lishe kwa wazazi pamoja na walezi ili waweze kuwapatia
watoto wao chakula mchanganyiko,hii itasaidia kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto"
Kauli hiyo imetolewa leo na Mganga mkuu wa Manispaa ya Iringa Dr.Jesca Lebba alipokuwa anafingua kikao cha kamati ya lishe kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa.
Dr.Lebba amesema,baadhi ya wazazi na walezi hawana uelewa wa kutosha katika masuala ya lishe hivyo kupelekea watoto wengi kuwa na udumavu.
Anzaeli Msigwa ni Afisa Lishe wa Manispaa ya Iringa anaainisha malengo ya kikao hicho kuwa ni kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji kulingana na mkakati wa Taifa unaotekelezwa ambao ulizinduliwa mwaka 2016 na utafanyiwa tathmini ifikapo mwaka 2021.
Msigwa anasema wanapitia taarifa za utekelezaji toka kwenye idara zinazounda kamati ya lishe ambazo ni idara ya Afya,Elimu,Kilimo,Maendeleo ya jamii,Mifugo na Mipango miji.
Amesema pia wanafanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali waliopo Manispaa ya Iringa kama,Lishe endelevu,Tahea,Nafaka,papa yohane wa 23 na nyingine.
Aidga wana pitia taarifa za utekelezaji za wadau hao kuona namna ambavyo malengo yamefikiwa au la, aliongezea
Wajumbe waliweka maazimio mbalimmbali ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutosha ya lishe ili kupunguza ama kumaliza kabisa tatizo la udumavu katika Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa