Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amewapongeza shirikisho la FIFA kwa kufika Iringa na kufanya mafunzo ya makocha kwa ngazi ya Chini (grassroot) yaliyofanyika kwa mfululizo wa siku Tano tangu tarehe 25 hadi leo wakihitimisha. Mafunzo hayo yakiwalenga zaidi vijana kuanzia miaka 6 mpaka 12
Mhe. Ngwada ameyasema hayo leo katika kufunga mafunzo hayo akiwatembelea eneo la Uwanja wa Samora ambapo mafunzo hayo yamefanyika akiwa ameambatana na baadhi ya waheshimiwa Madiwani wenzie.
Sanjari na hayo Mhe. Ibrahimu Ngwada ameendelea kuwataka washiriki hao kuzingatia ipasavyo mafunzo hayo na kwenda kuyatendea kazi ipasavyo kwa lengo kwa kuleta mabadiliko katika ulimwengu wa soko nchini hususani Mkoani Iringa na kusema kuwa anaamini hata timu zilizokufa basi nazo zitakwenda kusimama upya na vizuri.
Awali akiwasilisha taarifa ya mafunzo hayo Ndugu Adinani Chorobi, ambaye ni Katibu wa IRFA amesema katika fursa hiyo kumekuwa na changamoto ya muitikio mdogo kwa watu wa Iringa kwani washiriki wenngi wametokea Mikoa mingine, ambapo jumla ya washiriki 37 na kati yao mwanamke ni mmoja
Pia Ndg. Adinani Chorobi amemuomba Mstahiki Meya endapo fursa kama hiyozitajitokeza Halamashauri iwasaidie vijana wenye uhitaji ambao hawana fedha za kumudu gharama hizo za ushiriki wa mafunzo.
Na kwa upande wake Raymond Ngweba Mkufunzi kutoka FIFA ambaye ndiye anasimamia mafunzo hayo amewashukuru washiriki kwa kujitokeza kufanya mafunzo na anaamini watakwenda kuyafanyia kazi ipasavyo na pia amewataka kujitokeza tena awamu ya pili kwa mafunzo yatakayofanyika kwa ngazi ya juu zaidi
Naye Diwani wa Kata ya Mkimbizi mhe.Eliud Mvela ambaye aliwahi kushika nafasi za uongozi katika Shirikusho la Mpira Tanzania TFF hapo nyuma amewahasa washiriki hao wahakikishe wanazingatia mafunzo waliyopewa na wakayafanyie kazi ipasavyo kwa maendeleo ya soka la Tanzania, pia wahakikishe wanajiwekea mipango ambayo haitaruhusu wasio na vyeti kufundisha.
Akifunga mafunzo hayo Mhe. Ngwada ametoa ahadi kama Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kujitolea kushirikiana ipasavyo katika kila jambo ambalo litaletwa katika ofisi yake na Mkurugenzi ilikuhakikisha tunafanta vizuri katika sekta ya michezo katika Manispaa na Mkoa wa Iringa kwa ujumla.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa