Wakazi wa Kata ya Mkwawa wafurahia kushuka kwa gharama za umiliki ardhi kwa kiasi kikubwa kuanzia Julai Mosi 2023.
Akiongea kwenye moja ya mikutano ya madiwani inayoendelea kwenye Kata zote ndani ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Afisa Mipango Miji Ndg. Jonathan Mgeni amesema
“Kwa sasa gharama za kupata hati ya kiwanja zimepungua kwa kiasi kikubwa, kutoka shilingi elfu 50 hadi elfu 25 kwa hati moja”
Aidha ameongeza kwa kusema ada ya maombi ya umiliki wa ardhi imetoka elfu 20 hadi elfu 5 na pia upimaji wa viwanja umepungua kutoka shilingi laki mbili hadi elfu sitini mpaka sabini.
Diwani wa Kata ya Mkwawa Mhe. Amri Zakalia Kalinga amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kupunguza gharama za umiliki wa ardhi na shughuli za ujenzi kwa ujumla.
“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikia migogoro mingi inayohusu ardhi, hivyo namshukuru kwa niaba ya wananchi wa Kata yangu kwa kupunguza gharama za upatikanaji wa ardhi ili kila mwananchi aweze kumudu gharama hizo” Amesema Kalinga
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa