Naibu wazir wa Tamisemi Mhe. Dr. Festo Dugange amefanya ziara kwenye halmashauri ya manispaa ya Iringa na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile shule na vituo vya afya siku ya Jumatatu tarehe 18 Disemba, 2023 amabapo aliwapongeza wataalamu wa Manispaa Iringa kwa kazi nzuri za miradi wanavyoitekeleza, pia aliwasihi sana waache kuwa na miradi mingi ambayo haiishi kwa wakati kwani inakua haina faida na ni sawa na kupoteza tu hela za wananchi. Hivyo alimshauri Mkurugenzi pamoja na wataalamu wahakikishe wanamaliza mradi mmoja kwanza kisha ndo wahamishie nguvu kwenye mradi mwingine.
“Mkurugenzi hongereni sana kwa kazi nzuri mnazofanya za kusimamia na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwani hii inaonyesha mnamuunga mkono kwa vitendo Rais na hela anazoleta mnazisimamia vizuri saana.”
Aidha alitoa rai kwa wananchi wa Kitwiru waliokua wamekuja kumlaki naibu waziri alipofika kukagua mradi wa shule mpya ya kilongayena unaotelekezwa na ruzuku kutoka serikali kuu aliwaasa kushirikiana kwa pamoja na uongozi wa shule katika ulinzi wa miundombinu hiyo.
Wakati huo huo Diwani wa kata ya Mkimbizi Mhe. Eliud Mvela alimuomba mheshimiwa naibu waziri kusaidia upatikanaji wa umeme, barabara na maji katika eneo la Ugele Manyigi na Ilangila ambapo zahanati inajengwa. Mvela alisisitiziza upatikanaji wa huduma hizo kwani kwa kipindi kirefu wakazi wa eneo hilo ambao wapo ndani ya Manispaa wamekua wakipata adha kubwa.
“Mheshimiwa Naibu waziri tukijenga hii zahanati haitasaidia kama hakutakua na umeme, dawa zitaharibika kwani madawa mengi yanahitaji kuhifadhiwa sehem zenye ubaridi(majokofu) pia Mheshimiwa maji ni muhimu sana katika huduma za afya kwa ajili ya usafi kiujumla, alisema Mvela.”
Kwa upande wao wananchi wa Ugele walimshukuru Mheshiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio chao cha kuwajengea zahanati na kuwapelekea huduma aya umeme na maji, huku barabara ya kilometa 8 kwa kiwango cha changarawe kikiwa mbioni kutekelezwa.
Katika ziara hiyo ya siku moja Naibu waziri aliambatana na viongozi wa CCM Wilaya, wakiongozwa na Said Rubbeya, katibu Tawala Wilaya, timu ya management wakiongozwa na Mkurugenzi wa manispaa Iringa Ndugu Kastor Msigala.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa