Baraza maalum la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, limewakutanisha wadau mbalimbali wa Maendeleo katika kikao maalum cha tahmini ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri Novemba 7, 2022 kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa Mercy hall- Mlandege.
Mkutano huo uliongozwa na Mstahiki Meya wa Manispaa Mhe. Ibrahim Ngwada, huku wadau walio hudhuria ni pamoja na TARURA, CRDB , kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya, Rucu, na wengine.
Lengo la kikao hicho ni kutathimini maendeleo ya ukusanyaji wa mapato kwenye Halmashauri kupitia vyanzo mbalimbali vya mapato vilivyopo pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapato.
Aidha katika kikao hicho yalitolewa mapendekezo mbalimbali kutoka kwa Madiwani,wadau pamoja na wataalam ikiwa ni kutoa mkazo katika ukaguzi wa leseni pamoja na ushuru wa huduma (service levy) ili kuongeza mapato ndani ya Halmashauri na kuwatembelea wafanya biashara wote waliopo ndani ya kata zote kumi na nane (18) na kuwapa elimu ya kulipa kodi mbali mbali za Halmashauri.
Mapendekezo mengine ni Kutengeneza eneo la maegesho ya ma gari pamoja na shule za mchepuo wa kiingereza (English medium) zitasaidia kuongeza mapato, kuanzisha kwa sehemu ya kukutana viongozi na kubadilishana mawazo (Leaders club).
Kikao hicho kimeahirishwa kwa Mstahiki Meya kuwakaribisha wadau wote kuendelea kutoa maoni/mawazo yao kwa njia ya maandishi au kufika katika Ofisi yake iliyopo Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa