Mkuu wa Wilaya ya Iringa mh. Richard Kasesela amewaomba Wataalamu , Madiwani kwa kushirikiana na Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mh. Peter Msigwa kubuni vyanzo vipya vya Mapato ili kuboresha miundo mbinu na kuendeleza Miradi ya maendeleo katika jamii.
Mh. Kasesela ametoa wito huo katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Iringa kwa lengo la kupitisha mpango wa bajeti wa mwaka wa fedha 2018/2019.
Mbali na hayo Mh. Kasesela amewaomba Wataalamu wa Manispaa, Viongozi wa Dini pamoja na Viongozi wa Kisiasa kubuni mbinu mpya ya kutoa Elimu ya Ukimwi kwa Wananchi ili kuweza kupunguza ongezeko la Maambukizi ya Ukimwi Kimkoa hasa kwa kutoa Elimu katika Mikutano mbalimbali ya Kisiasa, Makanisani pamoja na Misikitini.
Kikao hiki cha Kamati ya Ushauri ya Wilaya (DCC) hufanyika kila mwaka kabla ya kupisha bajeti ya fedha ambapo hutoa Ushauri kwa Manispaa na kuipitisha kabla haijaenda Wizara ya fedha.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa