Kamati za kudumu za Halmashauti ya Manispaa ya Iringa zimewasilisha taarifa za utendaji kazi kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 katika Baraza la wazi la Madiwani lililofanyika juni 2 katika Ukumbi wa mikutano wa Manispaa .
Akizungumza katika Mkutano huo wa Baraza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amesema Manispaa imeendelea na ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ya Barabara, afya na Elimu, kwa lenngo la kuwaletea wananchi Maendeleo.
Mhe.Ngwada amesema Mradi wa ujenzi wa barabara ya Tumaini kwenda Igumbilo unaendelea vizuri na utakapokamilika utapunguza adha ya msongamano wa magari na kurahisisha shuguli za usafirishaji.
Pia ameipongeza Idara ya Fedha na biashara kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato na kushika nafasi ya 1 katika Halmashauri zote Nchini.
Pia ameipongeza Idara ya Elimu SekondariI kwa kung'ara, kushika nafasi ya kwanza (1) kimkoa katika matokeo ya kidato cha nne na kuwataka walimu kutokuridhika na matokeo hayo na badala yake kuongeza bidii ili kuleta matokeo mazuri zaidi.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe. Mohamed Moyo amewapongeza Madiwani na wataalam wa Manispaa ya Iringa kwa jitihada wanazozifanya katika kuwaletea wananchi maendeleo na ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya kuwashughulikia watumishi wote ambao wanaenenda kinyume na maadili ya kazi mara moja
Gerald Mwamuhamia, Kaimu Mkurugenzi amesema anapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Baraza na kuahidi kuyatendea kazi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa