Mkuu wa Mkoa wa Iringa,Queen Sendiga ametoa shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kupokea mgao wa shilingi bilioni saba milioni mia nane ambayo ni fedha kwaajili ya kupambana na ugonjwa wa UVIKO 19.
Akizungumza katika Mkutano na waandishi wa habari leo amesema fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa, jengo la watu mahututi,vyumba vya dharura pamoja na nyumba za watumishi.
“Ni vyema wananchi wa Iringa wakafahamu fedha hizi zinakwenda kufanyia nini lakini pia kama tunavyojua mwezi Januari tunatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule shikizi hivyo ujenzi utaanza muda sio mrefu”amesema Sendiga.
Aidha ametaja Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kama miongoni mwa Halmashauri zitakazonufaika na mgao huo wa fedha kwa kupatiwa bilioni 1.3 kwaajili ya ujenzi wa vyumba 69 vya madarasa huku Mufindi ikinufaika kwa kwa kupata bilioni 1.1 kwaajiliya vyumba 57 vya madarasa.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya kuanza kwa ujenzi unaotokana na fedha hizo pamoja na utaratibu ,amesema kuwa ujenzi huo unaruhusu kutumia wakandarasi au mafundi ujenzi lakini kwa kutumia kiwango cha fedha ile ile iliyopangwa katika mradi husika na kumalizika kwa muda uliopangwa.
Aidha Sendiga amesema wananchi wataendelea kushirikishwa na kuchangia katika shughuli hizo za ujenzi huku baadhi ya maeneo wananchi wakiwa tayari wameshaandaa maeneo kwaajili ya ujenzi wa miradi hiyo.
Sendiga amewataka wakurugenzi katika Halmashauri mbalimbali kusimamia vyema matumizi ya fedha hizo ili ziweze kutumika katika matumizi sahihi kama zilivyoelekezwa na kuhakikisha miradi iliyopangwa inatekelezeka kwa wakati.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa