Na Mwandishi Wetu, Iringa
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Selemani Jafo, ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kupanda miti ya matunda mashuleni na vyuoni ikiwa ni njia mojawapo ya kutunza mazingira na kunufaika na matunda.
Mhe. Jafo alitoa agizo hilo Januari 25, 2022 wakati wa uzinduzi wa kampeni ya upandaji wa miti ijulikanayo kama Soma na Mti uliofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Iringa.
Alitoa maelekezo kuwa asilimia 90 ya miti inayopandwa iwe ni ile ya matunda ili tuweze kupata matunda yakutosha yatakayosaidia kujenga afya zetu.
Kampeni hiyo ilizinduliwa kwa upandaji wa miti ya matunda ya parachichi,maua na vivuli ambapo Waziri Jafo aliongoza zoezi hilo akiambatana viongozi mbalimbali wakiwepo Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Mohamed Moyo, Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada.
Wengine ni Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mhe.Jesca Msambatavangu na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Kanda (Tfs) na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Iringa na wadau wa mazingira.
Katika zoezi hilo na jumla ya miche 305 ilipandwa na walimu, wanafunzi pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa