Mjumbe wa tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Thomas B Mihayo amewapongeza Wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Uchaguzi wa ngazi ya Jimbo na Kata, kwa kuteuliwa kwao kuwa watendaji wa Uchaguzi Mdogo unatarajiwa kufanyika 13 Julai 2023 Tanzania Bara.
Pongezi hizo amezitoa tarehe 19-06-2023 katika Ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliopo Manispaa ya Iringa wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa wasimamizi hao yanayofanyika kwa lengo la maandalizi ya Chaguzi ndogo za Madiwani katika kata 14 za Tanzania Bara.
"Kuchaguliwa kwenu hakukuja tu kwa kupitishwa, ila kumefanywa kwa mujibu wa Sheria lakini vilevile kwasababu mnastahili kuchaguliwa na mnastahili kuhudhuria mafunzo haya kama mlivyofanya."alisema Jaji.
Tume imepewa jukumu la kuratibu na kusimamia Uchaguzi katika ngazi ya Jimbo na Kata lakini matakwa ya kisheria yanaelekeza wawepo wasimamizi katika ngazi hizo kwa ajili ya kuendesha Uchaguzi kwa niaba ya Tume.
"Wote mliompo hapa mnafanya jukumu hili kwa niaba ya Tume, tume haiwezi kuwepo kila mahali hivyo imewateua nyinyi ili mfanye kwa niaba ya Tume, mkikosea nyinyi ndio Tume imekosea kwahiyo mjue mmewekwa kwenye sehemu nyeti saana."
Aidha amewaasa wale wanaosimamia Uchaguzi kwa Mara ya kwanza kuwa mategemeo yake na ya Tume kuwa watajifunza haraka na watapata uzoefu kupitia majadiliano ya pamoja na kwa wale wazoefu watatumia fursa hio kujiongezea maarifa mapya na kubadilishana uzoefu na washiriki wengine.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa