Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wa awamu ya nne, ambaye pia ni Mkuu wa Chuo kikuu cha Dar es salaam, Daktari Jakaya Mrisho Kikwete ameongoza tukio la utunuku wa vyeti kwa wahitimu wa chuo kikuu cha Dar es salaam tawi la Mkwawa kwenye mahafali ya 13 jana mwezi novemba 29 katika viwanja vya chuo kikuu cha Mkwawa
Aidha, Jakaya ameongozana na viongozi mbalimbali wa Serikali katika tukio hilo akiwemo Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Jesca Msambatavangu, Mtahiki Meya wa Manispaa Mhe. Ibrahim Ngwada pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndg. Herbert Bilia
Sambamba na hayo Mhe. Jakaya amewasihi wahitimu hao kwenda kuyatendea kazi ipasavyo yale waliyojifunza kwa muda wote walipokuwa chuoni kwa kuzingatia taaluma zao
Pia Mhe. Jakaya ametumia fursa hiyo kuwasihi watu wote waliokuwa eneo la tukio kutambua kuwa janga la UVIKO 19 bado lipo na linaendelea kuua hivyo wajiandae kikamilifu kwa wimbi la nne la ugonjwa huo kwa kuchukua tahadhari na kusema chanjo ni muhimu sana kwa ajili ya kinga dhidi ya ugonjwa huo hatari na kutoa funzo kupitia watu maarufu ambao wamekufa kwa ajili ya UVIKO amesema ugonjwa huu hauchagui.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa chuo Kikuu cha Dar es salaam Tawi la Mkwawa ndg. William Anangisye ameelezea mafanikio ya chuo hicho pamoja na changamoto ambazo zinakwamisha maendeleo ya chuo ni upungufu wa hosteli, kumbi za hadhara, na nyumba za walimu.
Aidha mwenyekiti amewasihi wahitimu wote kuwa na heshima na kufanya kazi kwa maadili kama waliyotoka nayo chuoni hapo kwani utii, bidii na kujituma ni njia ya mafanikio.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa