Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha RUCU leo 1/12/2020 wameadhimisha siku ya Ukimwi Duniani katika viwanja vya chuo kikuu hicho ambapo mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo alikuwa Katibu Tawala wilaya ndugu Estomini Sanga.
Ndugu Sanga ameiasa Jamiii kutokuwanyanyapaa wagonjwa wa ukimwi badala yake wanatakiwa kupendwa na kuwajali bila kuwabagua.
Aidha Sanga amesema katika siku hii ya ukimwi Duniani tunapaswa kukumbushana , kutafakari na kutatua changamoto mbalimbali dhidi ya janga hili la Ukimwi .
Jesca Lebba ni Mganga mkuu Manispaa ya Iringa amesema huduma za upimaji vvu zimetolewa bure katika viwanja vya Rucu kwa lengo la wananchi kufahamu hali zao za kiafya, hivyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupatiwa ushauri nasaha.
Lebba amesena huduma nyingine zilizotolewa katika viwanja hivyo ni pamoja na upimaji wa vvu, Elimu ya Ukimwi na kuchangia damu.
Maadhimisho hayo yalipambwa na burudani na michezo mbalimbali iliyotolewa na wanafunzi wa shule ya Msingi viziwi iliyoko Mtwivila.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa