Umoja wa wanawake Mkoa wa Iringa UWT leo 1/2/ 2021 wamefanya maadhimisho ya miaka 44 ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi katika viwanja vya Mwembetogwa ambapo pamoja na mambo mengine huduma ya upimaji afya kwa hiyari imetolewa bila malipo yeyote
Huduma zilizotolewa ni pamoja na upimaji wa virusi vya Ukimwi,Sukari,Saratani ya Mlango wa Kizazi, uchangiaji wa damu,Saratani ya matiti na Elimu ya lishe
Akiongea katika maadhimisho hayo mgeni rasmi Salim Abri amesema kazi iliyoko sasa kwa Chama Cha Mapinduzi ni kuwahudumia wananchi mara baada ya uchaguzi mkuu kupita
Aidha MNEC Ameshauri wakati mwingine kuwepo na utoaji wa Elimu ya uzazi pia Elimu ya lishe ili kuifanya jamii iepukane na maradhi mbalimbali
Abri amesema Watoto wakipata lishe bora watakua na afya njema kwani watasoma vizuri hivyo nashauri katika maadhimisho kama haya ufanyike utoaji wa Elimu ya lishe ili jamii iweze kuelimika na kuwa na afya bora
Pia ametoa wito kwa jamii kujitolea damu kwani imeelezwa kuwa chanzo kikubwa cha vifo vya akinamama wajawazito ni upungufu wa damu hivyo sadaka pekee tunayoweza kuitoa ni kuchangia damu kwa wale wenye uhitaji na jambo hilo linawezekana tukiamua.Tuchangie damu ili tuweze kuwa na Bank ya kutosha tuokoe maisha ya watanzania walio na uhitaji wa damu
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa