"Tunashukuru kwa Ujenzi wa Standi hii kwakuwa mpaka sasa, sisi vijana imetunufaisha kwa kujipatia kipato kwa ubebaji wa mizigo hivyo tunamshukuru Mh.Rais Magufuli kwa ujenzi huu" aliaema Joakhimu Fanueli mmoja wa vijana wanaojishughulisha katika stendi ya Igumbilo.
Bwana. Joakhimu ameyasema hayo katika ziara ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Ndugu Hamid Njovu, pamoja na Waandishi wa habari leo walipotembelea na kukagua katika eneo hilo.
Ikumbukwe kuwa leo ni siku ya pili ya ziara ya Ndg. Njovu inayohusisha kutembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea kutekelezwa ikiwa ni mafanikio ya miaka mitano ya Mh.Rais John Magufuli ndani ya Manispaa ya Iringa.
"Paulo Ngalawa ambaye ni Mwenyekiti mtaa wa ipogoro c amesema anafurahishwa na uwepo wa kituo cha watoto wenye mahitaji maalum kilichopo ndani ya eneo lake kwani kimekuwa ni msaada mkubwa kwa watoto hao.
Akiendelea kuzungumza Bwana Paulo amesema, kupitia mradi huo watoto walio wengi wenye matatizo ya akili hapo awali walionekana kuzagaa mitaani na kuonekana hawana umuhimu lakini mara baada ya kujengwa kwa kituo hicho kimesaidia kuwakusanya na kuwafundisha waweze kujitambua.
Aidha Miradi mingine iliyotembelewa siku ya leo ni pamoja na, ujenzi wa daraja la Tagamenda, Ujenzi wa shule mpya ya Sekondari eneo la Igumbilo, mradi wa maji wa ulonge, ujenzi wa vibanda vya biashara mlandege pamoja na Soko la kisasa la Mlandege.
Njovu amehitimisha ziara hiyo kwa kuwashukuru waandishi wa habari kwa kushirikiana nao katika ukaguzi huo wa miradi pia amewaomba kujenga mahusiano mazuri na waendelee kuitangaza Manispaa ya Iringa ndani na nje ya Mkoa kupitia shughuli zote za kimaendeleo zinazofanyika.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa