Kupitia kampeni ya nyumba ni choo wadau wa maendeleo Clouds Media kwenye kipindi cha XXL kwa kushirikiana na Smart fresh Toilet (SATO ) wametengeneza Masinki ishirini na tano (25) ya vyoo katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Manispaa ya Iringa (IRINGA GIRLS).
Ukarabati huo wa kubadili masinki ya vyoo shuleni hapo umeongozwa na mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela ambaye ametoa shukrani zake za dhati kwa menejimenti ya kipindi hicho iliyo chini ya B.dozen, na kampuni ya SATO kwa kuwezesha ukamilikaji wa mpango huo ambao utawawezesha wanafunzi kupata huduma bora za choo ili kuepuka magonjwa mbali mbali pia kuendana na kasi ya Rais Mh. John Pombe Magufuli.
Aidha wanafunzi kupitia kwa Dada Mkuu wa Shule ametoa shukrani za dhati kwa msaada huo walioupata shuleni hapo na kuahidi kusimamia utunzwaji wa masinki hayo ili huduma bora ya choo iendelee kupatikana kwa wanafunzi wote shuleni hapo.
XXL wamekaribishwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, ambapo
maadhimisho ya jiwe la mwezi (NYIMBO BORA PENDWA KATIKA MWEZI) yatafanyika Iringa katika viwanja vya Mwembetogwa na Msanii Nandy kutoka Tanzania House of Talent (THT) atatumbuiza kama mshindi kupitia nyimbo yake ya Kivuruge.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa