Baraza la Madiwani Halmashauri ya Manispaa ya Iringa leo tarehe 25/8/2022 limempitisha Mhe. Juli Sawani ambaye ni Diwani wa Kata ya Kihesa kuwa Naibu Meya wa Manispaa kwa mwaka mpya 2022/2023
Zoezi hilo limefanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Manispaa ya Iringa kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani la mwaka kujadili taarifa za utendaji na uwajibikaji wa Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2021/2022 huku likihudhuriwa na wananchi pamoja viongozi mbalimbali wa Chama cha Mapinduzi.
Akizungumza mara baada ya kuchaguliwa na kutangazwa kuwa Naibu Meya Mpya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Julius Sawani ambaye alishinda kwa kupata kura zote 26 za ndio,amesema yeye ni mtu wa kazi hivyo anaamini atamshauri vyema Mstahiki Meya katika kuhakikisha wanashirikiana kuleta maendeleo
Hata hvyo Mhe. Sawani ameendelea kuwataka watumishi na Madiwani kuonesha nidhamu nzuri kwa kila mmoja
Sambamba na hayo Mhe. Sawani amezitaka kamati mpya zilizoundwa kwa mwaka 2022/2023 zihakikishe zinasimamia vyema majukumu yake ili kuiletea Maendeleo Manispaa ya Iringa .
Naye Msthiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amewaomba wataalam na Madiwani pamoja na wajumbe wote wa Baraza kuwa na ushirikiano mzuri wa usimamizi wa miradi ya maendeleo kwa kipindi hiki cha mwaka mpya wa Serikali.
Hata hivyo Mhe. Ngwada amempongeza Mhe. Sawani kwa kuchaguliwa kuongoza katika nafasi ya Naibu Meya na kuwa anaamini watakwenda kushirikiana vyema kwa maslai mapana ya wananchi wa Manispaa ya Iringa.
Kwa upande wake Mhe.Jesca Msambatavangu ameitaka kamati ya Fedha na uongozi kutatua kero mbali mbali zinazoikabili Halmashauri kwa haraka ili kuepusha usumbufu kwa wananchi.
Katika Baraza hilo pia umefanyika uchaguzi wa wenyeviti na wajumbe wa kamati za kudumu za Halmashauri,ambapo Mhe.Eliud Mvela amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji na Mazingira Mhe.Maadhi Epautwa Mwenyekiti wa kamati ya Maadili,Mhe,Hellen Machibya Mwenyekiti kamati ya uchumi Afya na Elimu,na Naibu Meya Julius Sawani kamati ya kudhibiti ukimwi na Mfuko wa jimbo Mwenyekiti Mbunge wa jimbo la Iringa Mjini Mhe.Jesca Msambatavangu.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa