Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Omary Mkangama amepokea rasmi Barua za kujiuzulu kwa Madiwani wa kata ya Kwakilosa na Ruaha zilizopo manispaa ya Iringa.
Akitoa ufafanuzi wa kujiuzulu kwa Madiwani hao kwenye kikao kilichofanyika Siku ya Jumatano Tarehe 03/01/2018 ofisini kwake na Waandishi wa Habari, amewataja Madiwani hao kuwa ni Tandes Gabriel Sanga na Joseph Nzala Ryata Kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Aidha Mkangama ameeleza sababu walizozitoa za kujiuzulu kuwa ni kutoridhishwa na uongozaji wa Baraza la Madiwani na Mwenendo wa vyama vyao.
Barua za kujiuzulu kwa Madiwani hao zilipokelewa siku tofauti ambapo barua ya Diwani wa kata ya Kwakilosa ilipokelewa tarehe 29/12/2017 na Kata ya Ruaha ilipokelewa tarehe 03/01/2018.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa