Jumla ya miradi 7 ya maendeleo inayotekelzwa ndani ya Manispaa ya Iringa, imekaguliwa na Kamati ya Fedha na Uongozi ya Manispaa lengo likiwa ni kuona kushauri na kuboresha pale ambapo panahitaji marekebisho ili miradi hiyo itekelezwe kwa ufanisi mkubwa kabla ya kukamilika.
Miradi iliyopitiwa na Kamati ya Fedha na Uongozi ni Mradi wa Maji Ulonge, Kutembelea na kukagua mapokezi ya kidato cha kwanza Shule ya Sekondari Tagamenda sambamba na ujenzi wa madarasa, ujenzi wa madarasa matatu shule ya sekondari Ipogolo,kukagua ujenzi wa madarasa shule ya msingi mawelewele, kukagua eneo la maegesho ya magari nyuma ya soko la mashine tatu pamoja na kutembelea kituo cha television cha Manispaa yaani (IMTV).
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhesimiwa Alex Kimbe ambaye ni Meya wa Manispaa ya Iringa amesema, lengo la ziara ni kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuona maendeleo yake, kushauri, kurekebisha na kupongeza utekelezaji wa miradi hiyo.
Amesema ni muhimu kwa kamati kupitia miradi ya maendeleo kwani wananchi wapo kutaka kujua mafanikio hivyo wajibu wa waheshimiwa madiwa na watendaji wa Manispaa ni kuhakikisha kuwa miradi yote inatekelezwa kama ambavyo imepangwa na kwa ufanisi mkubwa ili kuweza kuleta maendeo kwa jamii ya watu wa Manispaa ya Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa