Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa na Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na uongozi Mhe.Ibrahim Ngwada amewataka Wataalam kusimamia Miradi ya Maendeleao inayoendelea kutekelezwa kwani kwa kufanya hivyo itapunguza changamoto za utekelezwaji wa miradi hiyo chini ya kiwango
Ngwada ameyasema hayo leo tarehe 20/8/2021 katika ziara ya kamati ya Fedha na Uongozi robo ya nne 2021 ambayo imefanyika kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali na kujionea maendeleo ya utekelezwaji wa miradi hiyo
Hata hivyo Ngwada ameagiza wataalamu wa Manispaa kusimamia miradi hiyo kwa kuzingatia taratibu zilizowekwa na kujenga miradi yenye ubora inayotakiwa,kukamilika kwa wakati pia iendane na thamani ya fedha zilizotolewa
Aidha katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Limbe B.Limbe alipata fursa ya kujitambulisha kwa wajumbe wa kamati hiyo na kuomba ushirikiano katika kuhakikisha wanaleta maendeleo kwenye Manispaa
Limbe amewashukuru wajumbe wa bodi za shule , zahanati pamoja na kamati za ujenzi kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa kwa kufika maeneo ya miradi hiyo kwani inaonyesha kuwa wao ni sehemu ya miradi hiyo
Katika ziara hiyo miradi iliyokaguliwa ni pamoja na ujenzi Kituo cha Afya Itamba,ujenzi wa bweni Shule ya Sekondari Mawelewele,ujenzi wa bweni shule ya Sekondari ya Nduli,na ujenzi wa madarasa 2 na choo Shule ya Msingi mnazi mmoja .
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa