Kamati ya kudhibiti Ukimwi ya Manispaa ya Iringa imefanya ziara ya robo ya tatu leo tarehe 3/5/2021 kukagua na kutembelea kikundi cha WAVIU cha Itika kilichopo Kata ya Mwangata kwa lengo la kuona shughuli za kiuchumi zinazofanywa na kikundi hicho.
Kikundi hicho kimeomba kupata mkopo kutoka Halmashauri ambao utawasaidia kuendesha mradi huo wa kuoka mikate na kukuza kipato chao.
Kikundi cha Itika kilipata msaada wa Mashine ya kuoka mikate yenye thamani ya shilingi milioni Arobaini na moja (41,000,000) kutoka kituo cha Allamano kwa lengo la kuwainua kiuchumi.Mashine hiyo ina uwezo wa kuoka wastani wa mikate thelasini na nane (38) au zaidi kulingana na ukubwa wa mikate kwa mara moja
Mhe.Kenyata Likotiko ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya Kudhibiti ukimwi amesisitiza Halmashauri kuwapa mkopo kwa wakati ili watimize malengo yao.
Kwa upande wake Ibrahim Ngwada Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa ambaye ni mjumbe wa kamati hiyo amezitaka Taasisi zingine zilizopo Manispaa ya Iringa zijitokeze kwa wingi kujitolea kusaidia vikundi vya WAVIU vilivyopo Manispaa ya Iringa ili iwepo nguvu ya pamoja kwani inaonyesha Taasisi zinazoshiriki kuchangia vikundi hivyo ni chache.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa