KAMATI YA MIPANGO MIJI NA MAZINGIRA YAKAGUA SHUGHULI ZA MAENDELEO MANISPAA YA IRINGA
Kamati ya mipango miji na mazingira imeishauri timu ya wataalamu Manispaa ya Iringa kuainisha maeneo ya wazi na wamiliki wa viwanja mbalimbali vyenye migogoro ili kuzuia uvamizi
Kamati imetoa ushauri huo katika ziara fupi ya kukagua miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu January-march 2018 ambapo miradi mbalimbali ilitembelewa ili kujua changamoto zinazoikabili miradi hiyo kwa lengo la kupata utatuzi
Aidha katika ziara hiyo kamati pia imetoa mapendekezo mbalimbali ikiwemo kupitia upya mikataba ya kodi ya pango kwa vibanda vya Halmashauri vilivyokodishwa kwa Wafanyabiashara ili kuokoa upotevu wa mapato
Ziara hiyo ilihususha wataalamu mbalimbali kutoka idara ya mipango miji ambapo maeneo mbalimbali yalitembelewa ikiwemo ukaguzi wa viwanja kata ya Igumbilo, kukagua ubadilishaji wa matumizi ya eneo la Kibwabwa, kukagua mchoro wa mipango miji Kitasegwa, kukagua urasimishaji wa eneo Isakalilo, kukagua Gereji ya Mlandege na Stendi pamoja na kukagua vibanda vya Halmashuri Mashine tatu.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa