KAMATI ya Siasa ya Halmashauri kuu ya CCM Wilaya ya Iringa Mjini ikIongozwa na Mawenyekiti wake ndugu Said Lubeya imefanya ziara ya siku mbili kutembelea na kukagua Miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Halmashauri ya Manispaa ya Iringa lengo likiwa kuona maendeleo ya miradi hiyo.
Ziara hiyo iliyofanyika Julai 10 na 11 2023 na kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi na Timu ya Menejimenti kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha kwa wakati uliopangwa na miradi hiyo ili ianze kutumika kwa manufaa ya wananchi
Lubeya amesema kazi ya kamati hiyo ni kuhakikisha Ilani ya Ccm inatekelezwa ili kuwapa nguvu ya kusimama majukwaani kwa ujasiri wakati utakapo fika wa kuomba ridhaa kwa wananchi kwa kipindi kingine.
'Wataalamu tumieni taaluma zenu vizuri hakikisheni fedha zilizotolewa na Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan zinatumika ipasavyo kwa maslahi mapana ya wananchi..
Nao wenyeviti wa Serikali za Mitaa wamekiri kushirikishwa vyema katika hatua zote za ujenzi wa miradi hiyo huku wakiomba Halmashauri ijenge Shule ya Sekondari Gangilonga na Kihesa kwani kuna idadi kubwa ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya Msingi katika Shule za Msingi Ngome,kihesa na Tumaini ambao wote wanaitegemea Shule ya Sekondari Kihesa na kufanya shule hiyo kuwa na msongamano wa wanafunzi hali ambayo inasababisha wanafunzi kushindwa kufanya vizuri katka mitihani yao ya mwisho.
Baadhi ya wajumbe walipata fursa ya kuuliza maswali katika maeneo ya Miradi ambayo yalijibiwa na timu ya Menejimenti iikiongozwa na Mkurugenzi ndugu Kastori Msigala.
Miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa vyumba 3 vya darasa Shule ya Msingi Lugalo ambapo walipokea tshs. 60,000,000/=,ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa na matundu 6 ya vyoo Shule ya msingi Ngome walipokea tshs. 137,000,000/=,ukamilishaji wa madarasa 3 Shule ya msingi Tumaini nao walipokea tshs.43,750,000/=,ukarabati wa jengo la OPD na ununuzi wa vifaa tiba zahanati ya Mtalagala walipokea tshs100,000,000/=
Miradi mingine ni ujenzi wa vyumba 5 vya madarasa Shule ya Asekondari Mtwivila walipokea tshs 100,000,000/=.
Kwa Upande wake Mkurugenzi ndugu Msigala amesema amepokea maelekezo yote kutoka kwenye Kamati hiyo na ameahidi kuyatendea kazi mara moja.
Ziara hiyo iliwahusisha vingozi mbali mbali i wa Chama na Serikali timu ya Menejimenti,ambapo Mwenyekiti wa Kamati hiyo aliwapongeza wajumbe kwa ushiriki wao katika ziara hiyo pamoja na michango waliyotoa iliyolenga kuboresha ujenzi wa Miradi hiyo ambayo inatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa