KAMATI YA SIASA YARIDHISHWA NA UTEKELEZAJI MIRADI-MANISPAA.
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Mjini imeridhishwa na ujenzi wa miradi inayotekelezwa Katika Sekta ya Afya, Elimu na Miundombinu katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa na kutoa rai kwa Menejimenti kuongeza kasi ya ujenzi wa miradi hiyo ili miradi yote ikamilike ifikapo Novemba 30 Mwaka huu.
Kauli hiyo imetolewa leo 06 Septemba 2024 na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Iringa Mjini Ndg, Said Rubbeya wakati kamati hiyo ilipotembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo kwa lengo la kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
" Msingi wa maendeleo yetu ni elimu, kama
elimu itapelekwa kimaarifa maarifa, hatutafikia malengo, tumekubaliana kuwa kila darasa wanafunzi wawe 45 na hili Mama Samia Suluhu Hassan Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataliweza. Niwapongeze sana Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi kwa kazi nzuri mliyofanya, madarasa yanavutia sana, sisi tumeridhika". Amesema Rubbeya alipokagua shule ya Sekondari Shabaha na Jengo la Kitega uchumi na huduma za jamii Welfare.
Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iringa Komredi Kheri James amesema amepokea maelekezo yaliyotolewa na Chama cha Mapinduzi CCM,kwani ndiyo dira na mwelekeo wa kuongeza ufanisi wa kazi, hivyo watafanyia kazi kwa haraka ili kukidhi matarajio ya wananchi na kujenga imani kwa Serikali yao.
Ziara hiyo ya Kamati ya Siasa wilaya ya Iringa Mjini ya Chama cha Mapinduzi CCM imefanikiwa kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ikiwemo ujenzi wa Zahanati ya Mtwivila, ujenzi wa miundombinu ya Hospitali ya Frelimo, ujenzi wa miundombinu shule ya Sekondari ya Kwavava, ujenzi wa jengo la kitega uchumi na huduma za jamii welfare, ujenzi wa barabara ya Old Dodoma kiwango cha lami, kuboresha barabara ya Kigonzile na ujenzi wa daraja na mingineyo.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa