Kamati ya uchumi Afya na Elimu inayoongozwa na Mheshimiwa Raphael Ngullo imefanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ambapo imekagua na kulembelea miradi mbalimbali ikiwemo, Eneo linalotarajiwa kujengwa Shule mpya ya Sekondari Kata ya Igumbilo, ujenzi wa Maabara na kituo cha kutolea dawa za kufubaza makali ya Virusi vya UKIMWI (ARV) katika kituo cha Afya Ipogolo, Vyumba vya Maduka katika Stendi ya Mabasi ya Mlandege, pamoja na eneo linalotarajiwa kujengwa Shule mpya ya Sekondari Kata ya Isakalilo.
Aidha kamati ilihitimisha ziara yake kwa kutembelea mradi wa ufyatuaji wa tofali katika Mtaa wa Ngelewala
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa