Mwenyekiti wa kamati ya UKIMWI Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Mhe. Kenyata Likotiko ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa amemtaka Mkurugenzi kuitazama zahanati ya Igumbilo kwa kuboresha na kuiongezea jengo la matibabu kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi
Likotiko ameyasema hayo leo Agosti 13 katika ziara yake na kamati hiyo iliyotembelea kituoni hapo kutazama namna shughuli za matibabu ya wagonjwa hao zinavyotolewa kutuoni hapo huku ikibainika changamoto ya ufinyu wa jengo kutokana na uwingi wa wanachi wanaohudumiwa katika kituo hicho
'Kituo hiki cha za zahanati ya Igumbilo kipo chini ya Manispaa ya Iringa hivyo ni muhimu jengo hili liboreshwe ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi alisema Likotiko'
Aidha ziara hiyo imetembelea na kukagua kituo cha Allamano kilichopo chini ya Taasisi binafsi ya CONSOLATA MISSIONARY SISTERS ambacho pia kinajishughulisha na kutoa huduma mbalimbali za ushauri wa kisaikolojia, elimu, malezi ma makuzi, uimarishaji uchumi na kaya na huduma za upimaji wa UKIMWI katika kujionea mwenendo wa utolewaji wa huduma za wagonjwa wa VVU
Likotiko ameupongeza uongozi wa Kituo hicho kwa namna wanavyoshirikiana na Manispaa kutekeleza majukumu yao kwa kutoa huduma bora kwa wakazi wa Manispaa ya Iringa
Omary Mkangama ni kaimu Mkurugenzi Manispaa amesema amepokea maelekezo yote yaliyotolewa na kamati na kuahidi kuyatendea kazi.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa