Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mhe.Ibrahim Ngwada amesema Halmashauri ina mpango wa kuingia ubia katika ujenzi wa jengo la kitega uchumi la Tembo bar karibu na standi kuu ya mabasi ya zamani.
Ngwada ametoa kauli hiyo katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili na kupitisha tararifa za kipindi cha robo ya tatu (Januari hadi Machi 2022/2023) ambapo amewakaribisha wananchi,Taasisi mbalimbali, na wafanyabiashara wenye nia wajitokeze ili kwa pamopa watekeleze mradi huo.
'Mkurugenzi, natambua kuna taasisi na wafanyabiashara wameanza kuonyesha nia mara baada ya kuona matangqzo yetu,Naagiza kasi ya matangqzo iongezeke ili tupate idadi kubwa ya waombaji na utekelezaji wa mradi huu uanze mara moja.alisema Ngwada.'
Katika hatua nyingine Ngwada amesisitiza suala la usafi wa Mazingira na kusema Manispaa imekuwa ikifanya vizuri kwenye mashindano ya usafi na kushika nafasi ya 1 na ya pili
Hivyo anasisitiza waongeze jitihada za usimamizi wa usafi katika maeneo yote kwa kuhakikisha wananchi wanafanya usafi na taka zinapelekwa dampo kwa wakati.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mhe.Veronica Kessy ameitaka Halmashauri kuhakikisha inakamilisha zoezi la kuwapanga machinga kwenye maeneo rsmi na kusimamia wale wanaorudi kwenye maeneo yqsiyo rasmi na kuwachukulia hatua.
Kessy amemshukuru Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa CCM ndugu Salim Abri ( ASAS) kwa ushirikiano wake mkubwa kutoa fedha za kujenga majengo ya kufanyia biashara machinga katika eneo la Mlandege na kusema amefanyq jambo kubwa ambqlo tunapqswa kumpongeza na kumshukuru.
NduguCharles Mwakalila ni kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa amesema ameyapokea maelekezo yote yaliyotolewa na Baraza la Madiwani na kuahidi kuyafanyia kazi.
Katika Baraza hilo jumla ya qgenda.10 zilijadiliwa ikiwemo kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha robo ya tatu kuanzia Januari hadi Machi 2022/2023 na maswali ya papo kwa papo kwa mujibu wa kanuni ya 24 ambapo waheshimiwa Madiwani walipata fursa ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi kutoka kwa Mstahiki Meya na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa.
Imeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Manispaa ya Iringa
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa