Mstahiki Meya Manispaa ya Iringa Mhe. Ibrahim Ngwada amewakaribisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kujitokeza kwa wingi kuwekeza ndani ya Manispaa ya Iringa katika maeneo mbalimbali ya sekta ya utalii
Aidha hayo ameyasema mbele ya baadhi ya waandishi wa Habari wanawake kutokea vyombo mbalimbali vya habari nchini, walipotembelea katika ofisi yake mara baada ya ziara yao ya siku moja walipotembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoani Iringa
Hata hivyo Mhe. Ngwada ameyataja maeneo mbalimbali ya uwekezaji ikiwemo eneo la Kihesa kilolo lenye hekta 220, lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa hoteli kubwa yenye hadhi ya Nyota tano litakalokuwa na maduka makubwa, kumbi za kisasa za mikutano, zahanati, kambi za kupumzikia watalii kwenye eneo la utalii la jiwe gangilonga
Mhe Ngwada amesema mikakati hiyo imefanyikika kwa kuzingatia Mkoa wa Iringa ndio kitovu cha utalii nyanda za juu kusini ambapo maonesho ya utalii hufanyika kila mwaka na Mkoa huu ndio mwenyeji wa maonesho hayo.
Bi.Tatu kunambi ni Afisa Mipango Miji wa Manispaa ya Iringa amesema katika eneo la kihesa kilolo Halmashauri imeandaa michoro ya majengo yatakayojengwa pindi wawekezaji watakapojitokeza ambayo ni ujenzi wa Hoteli kubwa yenye hadhi ya Nyota tano,ujenzi wa maduka makubwa (shopping malls) ujenzi wa viwanja vikubwa vya michezo kwa watoto na watu wazima,ujenzi wa kituo cha Afya ,ujenzi wa kumbi za kisasa za mikutano na eneo la maegesho ya magari.
Mary Mwakibete ni Mkurugenzi wa Bete TV na Mratibu wa ziara ya waandishi wa habari wanawake amesema wameanzisha kampeni ya kutembelea vivutio vya utalii na kuibua fursa za uwekezaji zilizopo katika Mikoa yote nchini Tanzania, lengo ni kuwa mabalozi wazuri kwa kuzitangaza na kuhamasiha jamii kujitokeza kutembelea vivutio vyetu na pia kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana katika kila Mkoa. Huku kauli mbiu ikiwa ni 'TALII WEKEZA TANZANIA.'
Jumla ya waandishi wa habari 31 kutoka vyombo mbalimbali vya habari walitembelea hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo Mkoa wa Iringa na kujionea namna hifadhi hiyo ilivyorikiwa kwa kuwa na wanyama aina mbalimbali wakiwemo Tandala wakubwa na wadogo na kujifunza tabia mbalimbali za wanyama hao.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa