Katika kuadhimisha siku ya usafi duniani wafanyakazi wa Manispaa ya Iringa pamoja na wadau mbalimbali wa mazingira Wamefanya usafi katika hospitali ya wilaya Frelimo.
Akizungumza katika tukio hilo mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard Kasesela amesema "Usafi unaanza na wewe mwenyewe kisha unafuata usafi wa mazingira, tulichokifanya leo ni jambo la kuigwa na ninaomba liwe endelevu tusiwe na tabia ya kufanya usafi siku ya mazingira tu".
Kwa upande wake kiongozi kutoka Envbright, kikundi cha usafi Ndg. Paulo Myovela amesema ni jukumu la kila mmoja kuhakikisha mazingira yanakuwa safi ndio maana wao kama wadau wa mazingira wameamua kuungana na wadau wengine kuhakikisha kuwa Iringa inazidi kung'ara na kuwa safi.
Usafi huo umefanywa na wafanyakazi wa Manispaa ya Iringa (MWAKIMC), Nipe Fagio, Envibright, Elena foundation, Raleigh intenational, wafanyakazi wa hospital ya Frelimo, Wanafunzi wa scout kutoka Isimila Sekondari pamoja na wananchi wa Manispaa ya Iringa .
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa