"Angalieni namna ya kuwagawia wafungwa waliopo Iringa Manispaa,na Halmashauri ya wilaya ya Iringa vyandarua ili kuwakinga na ugonjwa wa malaria."
Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa Wilaya ya Iringa mh. Richard Kasesela katika ukumbi wa chuo kikuu Huria alipokuwa akizindua rasmi kampeni ya ugawaji wa vyandarua katika jamii.
Mh.Kasesela amewataka waratibu kuwa makini wakati wa utekelezaji wa
zoezi hilo kuanzia usajili wa kaya hadi ugawaji wa vyandarua ili kusiwepo na dosari yeyote itakayojitokeza.
Pia ameshauri zoezi hilo kufanyika mapema kabla ya mwezi wa nane (8)ili kuilinda jamii na ugonjwa wa malaria ambao ni hatari kwa afya hasa kwa kina mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.
Awali kaimu Mkurugenzi Maniapaa ya Iringa ndugu Omary Mkangama akimkaribisha mgeni rasmi amewataka wanufaika kupewa elimu sahihi ya matumizi ya vyandarua hivyo kwani inaonyesha baadhi ya wananchi wamekuwa wakibadili matumizi na kufanyia shughuli zingine kinyume na matumizi kusudiwa.
Mkangama ameitaka timu itakayoenda kwenye kaya kuhakikisha wanawatendea haki wananchi na kutumia mafunzo waliyopewa kufanya kazi hiyo kwa weledi.
Uzinduzi huo umewashirikisha wataalamu kutoka wilaya mbili wakiwemo waganga wakuu wa wilaya
,Maafisa mipango ,wachumi,viongozi wa dini,
timu ya uendeshaji wa huduma za afya,pamoja na maafisa maendeleo ya jamii huku mada mbali mbali zikitolewa na wataalamu toka Wizara ya afya ikiwa ni pamoja na Hali halisi ya ugonjwa wa malaria katika Mkoa wa Iringa.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa