Mkuu wa wilaya ya Iringa Mh. Richard kasesela wakati akiongea na wafanyabiashara wadogo wa maeneo ya Stendi ya zamani ya Mabasi, Miyomboni pamoja na Mashine tatu ametoa wito kwa wataalamu kutofanya msako wowote katika maeneo ya wafanyabiashara wa dogo bila kufuata utaratibu.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya wataalamu wa NEMC kutoka Ofisi za Kanda Nyanda za Juu Kusini pamoja na TBS makao Makuu waliodaiwa kutokea kuvamia soko la mshine na kuanza msako wa vifungashio vyepesi imedaiwa kuwa hawakufata taratibu zilizowekwa na uongozi wa soko na kutowatendea haki kwa kuwanyang,anya vifungashio walivyodai havijakidhi vigezo.
Mbali na kero hiyo pia wamelalamikia baadhi ya askari kutokuwa na lugha nzuri pindi wanapofika sokoni hapo kutimiza majukumu yao.
Aidha Mh. kasesela amehidi kuzifanyia kazi kero zao ikiwa ni pamoja na kuzuia wataalamu kufanya oparesheni bila kutoa elimu husika kwa wajasiliamali hao.
Awali akitoa malalamiko yake mwenyekiti wa soko la mashine tatu amesema viiongozi wa soko wamekuwa wakidharauliwa kwani baadhi ya wataalamu wanavamia sokoni hapo bila taarifa na kuanza ukaguzi jambo ambalo linaweza kuleta uvunjifu wa amani.
Iringa Municipal Council
Sanduku la Posta: 162
Telephone: +255-2702647
Mobile: 255-2702647
Email: md@iringamc.go.tz
hakimiliki@2017Iringa Manispaa haki zote zimehifadhiwa